11/11
2009

Muhtasari wa Sera na Sheria za Ardhi na Maliasili

Serikali huhitaji kuwa na mpango wa utekelezaji, unaojulikana kama Sera. Sharia husika zinatumika kusimamia utekelezaji wa sera na kuzisaidia kulinda ipasavyo rasilimali muhimu kama ardhi, misitu na wanyamapori. Kuna tofauti muhimu kati ya Sheria na Sera. Sera inazungumzia: i) Mipango ya Serikali kwa sekta mbalimbali, kama vile ardhi, elimu, afya, kilimo n.k. ii) Namna Serikali itakavyotekeleza mipango yake iii) Kuweka wazi sheria na kanuni zinazopaswa kudhibiti utoaji uamuzi.
Ni Sheria na wala si Sera ambazo ndizo zinaelekeza haki muhimu, mamlaka na wajibu katika kudhibiti utekelezaji wa sera kama ya ardhi na rasilimali. Sheria zinafafanua namna ya kutekeleza sera na pia:
- Kuamua ni asasi zipi na wahusika wenye haki na mamlaka ya kutoa maamuzi
- Zinaeleza adhabu inayotolewa kwa kuzivunja sheria na kanuni
- Kuzisaidia mahakama kuhimiza utekelezaji

Full Document:

AttachmentLNR-Swahili.pdf